MABORESHO USIMAMIZI WA ELIMU
      Home
TAMISEMI YABORESHA USIMAMIZI WA ELIMU NCHINI | CHUO CHA HOMBOLO CHAPATA MAFANIKIO (NA FRED KIBANO)
   
Utangulizi
 
Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe mnamo tarehe 12 Februari, 2008 alitoa Tamko kuhusu kugatua Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Sekondari kutoka Wizara ya Elimu kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 
Bw.Benard Makali Mkurugenzi wa Uratibu wa Elimu TAMISEMI aliwasilisha mada kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu Bwa. Jumanne Sagini wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa Wabunge wa Kamati ya OWM TAMISEMI alieleza sababu za Serikali kufanya mabadiliko katika elimu ya Sekondari lengo kuu likiwa kupeleka huduma karibu na walengwa. Huduma hizo ni pamoja na malipo ya mishahara, kupandishwa vyeo, stahili mbalimbali za walimu, ujenzi wa Miundombinu ya shule na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
 
Ugatuaji ukihusisha mchakato mzima wa kuhamisha majukumu ya kupanga, kutoa maamuzi, kusimamia rasilimali na utekelezaji kutoka ngazi za juu kwenda ngazi za chini. Hii inahusisha kuhamisha majukumu kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa. kuleta mafanikio katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali, kuleta ufanisi, usawa na demokrasia.
 
Awali kabla ya ugatuaji mazingira ya utoaji elimu ya sekondari yalionesha kuwepo kwa ongezeko la Shule za Sekondari kutoka shule 1,291 (2004) hadi 3,798 (2008) na hadi Machi, 2013 zilifikia shule 4,644 sawa na asilimia 359.7
 
Kutoka mwaka 2004, idadi ya walimu wa shule za sekondari za Serikali iliongezeka kutoka 11,320 (2004) hadi 32,835 (2008) na hadi Machi, 2013 wapo walimu 63,415 sawa na asilimia 560. Idadi ya wanafunzi iliongezeka kutoka 401,598 (2004) hadi 1,222,403 (2008) hadi Juni, 2012 idadi ya wanafunzi ilifikia 1,884,272, sawa na asilimia 154.
 
Matokeo ya Kuongezeka kwa Elimu ya Sekondari ni pamoja na Usimamizi wa moja kwa moja kutoka WEMU ambao ulikuwa mgumu, Kulikuwepo ucheleweshaji wa utoaji wa huduma, Ubora wa huduma zilizokuwa zinatolewa ulipungua, Walengwa walikuwa mbali na watoa maamuzi na Jamii kukosa nafasi ya umiliki wa shule katika maeneo yao.
 
Kipindi cha Julai 2009, OWM TAMISEMI ilikabidhiwa rasmi majukumu ya Usimamizi, Uratibu na Uendeshaji wa Elimu ya Sekondari kwa kuzingatia sheria na taratibu hizo. Mwezi Julai 2011 Divisheni ya Uratibu wa Elimu TAMISEMI ilianza kazi madhumuni yakiwa Usimamizi madhubuti, Ufuatiliaji, Uratibu na kuhakikisha kuwa Ugatuaji wa majukumu ya Elimu yaliyopelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yanatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.
 
Shule za Msingi na Sekondari zimepata mafanikio mbalimbali ambayo ni pamoja na Walimu wapya kulipwa mishahara, posho ya kujikimu na nauli kwa wakati, Fedha za chakula cha wanafunzi kutolewa kwa wakati, na Chakula cha wanafunzi kinachotolewa katika shule za bweni kimeboreshwa.
 
Pia kupungua kwa migomo ya wanafunzi inayosababishwa na ukosefu wa huduma bora ya chakula, maji, umeme na vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Utoro kwa walimu kudhibitiwa kwa urahisi kwa Halmashauri kuzuia mishahara inapogundulika kuwa hawapo katika maeneo ya kazi,
 
Matumizi mazuri ya wakati kwa Wakuu wa Shule na walimu kwani wanabakia muda mrefu vituoni, na Kuboresha kiwango cha taaluma kwa kuokoa muda uliokuwa ukipotea kwa walimu kufuatilia masuala yao Wizara ya Elimu Makao Makuu Dar es Salaam .
 
 
Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari zina kabiliwa na changamoto kama vile Kuchelewa kwa mchakato wa uhuishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 1995, Sheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 na Marekebisho yake ya Mwaka 1995; na Sheria Na 7, 8 & 9 za Serikali za Mitaa za mwaka 1982 na Marekebisho yake ya mwaka 2000 ili kuendena na ugatuaji wa Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Sekondari kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 
Aidha, Uteuzi wa Wakuu wa Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari bado unafanywa na Katibu Mkuu WEMU tofauti na Idara zingine kwenye MSM, unasababisha mkanganyiko katika kusimamia uwajibikaji kati ya WEMU na OWM TAMISEMI, Ukosefu wa usafiri katika ngazi ya Halmashauri katika Idara ya Elimu ya Msingi na Sekondari.
Vilevile, katika baadhi ya Shule za Sekondari na hasa za bweni. Hata zile zenye magari inaonyesha magari hayo ni chakavu, Miundombinu chakavu katika baadhi ya shule za kutwa na za bweni (madarasa na nyumba za walimu, mabomba ya maji na maabara) kwa Msingi na Sekondari, Uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Upungufu wa walimu hususani katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha, na pia Baadhi ya Walimu kutopenda kufanya kazi kwenye mazingira ya vijijini.
 
Mikakati iliyopendekezwa kukabiliana na changamoto hizo ni pamoja na Kutenga bajeti ya elimu kwa kuzingatia vipaumbele, Kutumia kwa uangalifu na kwa usahihi ruzuku ya uendeshaji na ruzuku ya maendeleo, Kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia hasa vijijini yawe na vivutio kwa walimu kuweza kukubali kufanya kazi katika maeneo husika,
 
  Serikali kuwezesha usajili wa wanafunzi wengi kujiunga na Vyuo vya Ualimu na hatimaye kupata idadi kubwa ya walimu wanaofuzu mafunzo ya ualimu katika ngazi ya Msingi na Sekondari, Kushirikisha wadau mbalimali wa elimu katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za usimamizi na uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari, na vilevile Kuendelea na utaratibu wa mikutano ya Kamati Kazi ya Ugatuaji na Usimamizi za WEMU na OWM-TAMISEMI ili kuimarisha Uratibu wa Elimu.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bw.Muriri J.Joseph amesema mbali na mafanikio waliyopata kuna changamoto kadhaa zikiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri kupeleka watumishi wao chuoni hapo lakini hawalipi ada na kufanya uendeshaji wa chuo kuwa mgumu,
Pia Serikali kupeleka fedha kidogo chuoni hapo kwa ajili ya kulipia deni la Mfuko wa pensheni wa LAPF ambao ndio umjenga majengo kadhaa kattika chuo hicho, na vilevile ubovu wa barabara ya kilomita 26 kutoka Ihumwa kwenda Hombolo.
Wakichangia maendeleo na changamoto za chuo cha Hombolo na Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya OWM TAMISEMI wakati wa mafunzo waliyopata chuoni hapo wamesema Waziri Mkuu wa Tanzania mhe. Mizengo Pinda amekwisha ahidi kujenga barabara ya kiwango cha lami kutoka Ihumwa kwenda Hombolo.
 
Lakini pia matumizi ya TEHAMA yatumike ili kuondoa tatizo la vitabu na walimu kama inavyofanya vyuo vingine Duniani.
 
Akihitimisha mafunzo hayo Mhe. Kassim Majaliwa Naibu Waziri wa nchi TAMISEMI (E) alisema anaandaa utaratibu viwanja vya Hombolo vitumike kwa ajili ya michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA ili kuvipa hadhi viwanja hivyo ambavyo ni vizuri na vinakidhi viwango vya kimataifa