Click on the slide!

Kiapo

Picha: Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia (Mb) kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Mhe.Ghasia amechukua nafasi ya Mhe. George Huruma Mkuchika (Mb) ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala bora.

Click on the slide!

Karibu Mh. Waziri

Picha: Pmoralg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia (Mb) akiwa na Naibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Waheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) na Aggrey Mwanri (Mb) mara baada ya kukaribishwa rasmi katika Ofisi ndogo ya Wizara hiyo iliyopo jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Katibu Mkuu bw. Hussein Kattanga, Naibu Makatibu Wakuu bw. Jumanne Sagini na Alphayo Kidata na baadhi ya watumishi wa Wizara.

Click on the slide!

Makatibu Tawala Wapya wa Mikoa

Picha: Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wapya wa Mikoa mara baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo hivi karibuni. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Mhe.Dk.Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia (Mb).

Click on the slide!

Wakuu Wapya wa Mikoa

Picha: Pmoralg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa wapya mara baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo hivi karibuni. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Mhe.Dk.Mohamed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda (Mb).

Click on the slide!

Jeong-Sam Kim

Picha: Pmoralg

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bw. Jumanne Abdallah Sagini akimkabidhi zawadi ya kalenda ya TAMISEMI Rais wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LOGODI) cha Korea Kusini bw.Jeong-Sam Kim wakati Rais huyo alipotembelea Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo kilichopo mjini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo bw. John Joseph Muriri.

Frontpage Slideshow (version 1.7.2) - Copyright © 2006-2008 by JoomlaWorks
Album: Picha Mbalimbali
Other Galleries          
© 2013 PMORALG