Description:
Kutokana na Maafisa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kutokuwa na Ofisi maalum za kufanyia kazi, imepelekea kupungua kwa ufanisi wa utendaji kazi katika ngazi hizo. Hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imependekeza ramani zilizoambatanishwa kutumiwa na Halmashauri kujenga Ofisi za Maafisa Watendaji. Halmashauri inaweza kujenga Ofisi bora zaidi ya hii kulingana na uwezo wao kifedha kuzingatia vigezo vya ramani zilizoambatanishwa.
Ilikuweza kusoma ramani hii lazima komputa yako iwe na Programu za 'AutoCAD' na 'WinZip'.