Contact   |   Site map  


 

 
 

TAMISEMI YAALIKWA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Date: 16th Oct 08
12:00am - 12:00am
Location: Musoma
Contact Person: IEC UNIT
Contact Telephone:
Attached Document:



Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itakuwa miongoni mwa Wizara za Kisekta ambazo zimepangwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa tarehe 16 Oktoba mjini Musoma mwaka huu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Stephen Wasira.

Katika kuadhimisha siku hiyo ambayo kauli mbiu yake ni changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi ya nishati itokanayo na vyakula, Ofisi ya Waziri Mkuu- Tamisemi kupitia Idara ya Uratibu wa Kisekta ambayo pamoja na mambo mengine itahusika na kuandaa hotuba ya mgeni rasmi.

Kutokana na Wizara hiyo kuwa ndiyo Msimamizi mkuu wa halmashauri nchini mbali na kuandaa risala hiyo pia itahusika katika kuzisaidia halmashauri nchini kuboresha mipango yake ya kilimo na mifugo.

maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanafanyika tarehe 16 oktoba mwaka huu wakati dunia ikishuhudia kupanda kwa gharama za chakula ambapo maeneo yaliyo masikini ndiyo yaliyoathirika zaidi na upungufu huo.

Mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati ya mafuta inayotokana na mimea imechangia kwa kiasi kikubwa hali hii.


 
  October 2008  
S M T W T F S
      1 2 3 4
5 6 7 8 9 10 11
12 13 14 15 16 17 18
19 20 21 22 23 24 25
26 27 28 29 30 31  

<< back to list of events.