Contact   |   Site map  


 

 
 

Current

UHAMISHO - DISEMBA 2009

1.0  Utangulizi


Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imeendelea na utaratibu wake wa kushughulikia maombi ya uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mwezi Juni na Disemba kila mwaka.


2.0  Uhamisho wa Disemba, 2009


Katika kipindi kinachoishia Disemba 2009, jumla ya maombi 1399 ya uhamisho wa watumisho wa kada mbalimbali yamepokelewa na OWM-TAMISEMI.


3.0  Muda wa kufuatilia majibu


Waombaji wanashauriwa kufuatilia majibu ya maombi yao, kupitia ofisi za Wakurugenzi wao kuanzia wiki ya pili ya mwezi Januari 2010. Kwa maoni na ufafanuzi tafadhali tuma barua pepe kupitia ps@pmoralg.go.tz.


Aidha taarifa za Maombi ya Uhamisho wa Watumishi zitapatikana katika Tovuti za Mikoa pamoja na mbao za matangazo kwenye Ofisi za Wakuu wa Mikoa na pia katika katika Tovuti ya OWM-TAMISEMI, www.pmoralg.go.tz .


OWM – TAMISEMI INAWASHUKURU WATEJA WOTE KWA USHIRIKIANO



Document : taarifa_waliokidhi_utangulizi.pdf





Posted: 4th Mar 10 by Hellen Macha
<< back to list of News.