Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI juzi walichanga zaidi ya shilingi milioni 8.7 kwa ajili ya kuwasaidia zaidi ya wakazi 22,000 wilayani Kilosa ambao wamekumbwa na mafuriko.
Katika harambee hiyo iliyofanyika wakati wa hafla ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2010 na kuwaaga watumishi wastaafu wa TAMISEMI Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mheshimiwa Celina Kombani aliwaongoza watumishi wa Ofisi yake katika kuwachangia waathirika wa Mafuriko Wilayani Kilosa.
Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi laki saba fedha taslim zilipatikana na nyingine milioni 8 zitachangwa na Idara 8 za Wizara hiyo.
Mheshimiwa Kombani aliwataka Watumishi wa TAMISEMI na Watanzania kuungana na Wananchi wa Kilosa kwa kuwachangia chochote kile wanachokiweza kutokana na mazingira magumu ambayo wananchi hayo wanakabiliana nayo hivi sasa.
Alisema athari za mafuriko zimesababisha maelfu ya wananchi wilayani humo kuishi katika mazingira magumu. Aliongeza kuwa japo wananchi wa Kilosa wameathirika na mafuriko hayo lakini mvua nyingi zimenyesha mkoani Dodoma na kusababisha maji kujaa wilayani humo.
Posted: 1st Mar 10 by IEC UNIT
|