Contact   |   Site map  


 

 
 

Current

TAMISEMI YAADHIMISHA SHEREHE ZA MAPINDUZI KWA KUPANDA MITI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Celina Kombani tarehe 12 januari mwaka huu aliwaongoza zaidi ya watumishi 300 kutoka TAMISEMI na Manispaa za Dodoma na Chamwino kupanda miti 1200 katika eneo la Mlimwa lililopo mjini Dodoma.

Waziri Kombani alieleza kuwa ni azma ya TAMISEMI kuendelea na utamaduni wake wa kupanda miti kila tarehe 12 januari ya kila mwaka kwa lengo la kuung’arisha mji wa Dodoma na miti ya kila aina.

Mwaka jana zaidi ya miti 1000 ilipandwa na Watumishi wa TAMISEMI katika eneo la Iyumbu ambalo lipo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Waziri Kombani alisema kuwa lengo la Wizara yake ni kuhakikisha kuwa Manispaa ya Dodoma inapendeza kwa kuzunguukwa na miti, na kuahidi kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Alitumia fursa hiyo kuzitaka Manispaa na Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya kupanda miti kila mwaka ili kuepusha athari zitokanazo na jangwa.

Naye Mratibu wa zoezi hilo la Upandaji miti bwana Francis Sekibaha alisema kuwa mwaka huu TAMISEMI imepanda miti 1200, mwaka jana ilipandwa miti 1000 na anatarajia kuwa zaidi ya miti 2000 itapandwa mwakani.

Mbali na waziri Kombani, zoezi la kupanda miti pia liliwashirikisha Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI bwana Abdallah Jumanne Sagini, Meya wa Manispaa ya Dodoma, Francis Mazanda, na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino.

 







Posted: 1st Mar 10 by IEC UNIT
<< back to list of News.