Contact   |   Site map  


 

 
 

Current

KIBAHA YATIMIZA MIAKA 40 KWA KUMUENZI HAYATI MWALIMU NYERERE

Shirika la Elimu Kibaha hivi karibuni limetimiza miaka 40 kwa kumuenzi Baba wa Taifa, ambaye alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa shirika hilo linaongoza vita dhidi ya maadui ujinga, maradhi na umasikini


Akieleza mchango wa hayati Baba wa Taifa wakati wa  sherehe hizo za miaka 40, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Elimu Kibaha kanali Mstaafu Ferdinand Swai alisema kuwa Mwalimu alilipenda Shirika kwa sababu kuu 3.


Kanali Swai alizitaja sababu hizo kuwa ni azma ya Mwalimu kuona kuwa Shirika ni kituo cha kuleta maendeleo vijijini, Shughuli za Shirika zinaendeshwa kwa kushabihiana na kushabikiana, Shirika ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi za ‘Nordic’.


Nchi za Nordic kwa kugharamia Mradi na kutoa wataalamu walioendesha Mradi na hatimaye kuukabidhi kwa Serikali ya Tanzania kama ilivyokusudiwa.

Serikali za awamu zote kwa kuendelea kulidumisha Shirika pamoja na mabadiliko ya hali ya uchumi na sera za nchi yetu.


Wenyeviti wa Bodi na Wajumbe wa Bodi zote kwa miongozo na maelekezo yao ya mara kwa mara viliwezesha Shirika  kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Wakurugenzi Watendaji na Manejimenti yote ya Shirika kwa kazi zao walizofanya.

Wafanyakazi wote wa Shirika waliostaafu na ambao bado wako kazini kwa moyo wao wa kujituma na mshikamano   katika kufanya kazi za Shirika. Wadau wengine wote (orodha ni ndefu) kwa ushirikiano wao.

 



Document : taarifa ya mkurugenzi kec.doc





Posted: 1st Mar 10 by IEC UNIT
<< back to list of News.