Wananchi wa Vijiji vya Nyamisati na Nyanjati Wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani wametakiwa kuulinda Msitu wa asili unaozunguuka vijiji hivyo ili uweze kuleta manufaa kwa taifa.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mratibu wa PFM nchini bwana Francis Sekibaha wakati alipotembelea Misitu miwili ya ya hifadhi ya Kikale na Mchungwa, ambayo imezunguukwa na vijiji sava na inapakana na pwani ya bahari ya hindi. Mratibu huyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI aliwataka wananchi wa vijiji hivyo kuulinda na kuuhifadhi vema Msitu huo wa asili kwani huwaletea Mvua, na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Picha hii inaonyesha Msitu uliojifunga wa Mikoko iliyofungamana vizuri uliopo Kijiji cha Nyamisati Wilayani Rufiji.
Nao Wakazi wa Nyamisati ambao wengi wao ni Wavuvi waliiomba Serikali iwasaidie vifaa kama Viatu na sare ili ziwawezeshe wananchi wanaolinda Msitu huo ambao ni Skauti kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa.
Mapema Mratibu wa PFM Wilayani Rufiji bwana Donath Nambua alisema kuwa Misitu hiyo ilianza kuhifadhiwa toka mwaka 1930. hata hivyo tangu ilipotangazwa kipindi chote hicho Misitu hiyo ilikosa usimamizi.
Alisema mwaka 2006 wananchi waliitikia wito wa kusimamia ulizni wa Misitu hiyo ambayo mbali ya kuwa na wanyama wa kila aina pia ina miti mingi aina ya Mikoko.
Aliongeza kuwa siri kubwa ya mafanikio ya kuilinda misitu hiyo ni kuwepo kwa kamati imara ya mazingira ambayo ina wajumbe kati ya 9 na 15.
Kutokana na kukabiliana vema na changamoto za uchomaji ovyo moto na ukataji miti Misitu hiyo imeweza kuongeza Uoto wa asili na maji hasa kwenye maeneo yaliyokuwa wazi ndani ya msitu.
Posted: 4th Mar 10 by IEC UNIT
|