Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwaarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 21 hadi 23 Machi, 2012 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Document : tangazo kuitwa kazini usaili wa tarehe 16 hadi 17 februari, 2012 - arusha technic
Posted: 30th Apr 12 by GC UNIT
|